Urusi yajibu mapigo, yamuwekea vikwazo Rais Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais wa Urusi, Vladimir Putin
NCHI ya Urusi imemuwekea vikwazo vya kuingia nchini humo Rais wa Marekani, Joe Biden na maofisa wengine 12 wa Taifa hilo, ikiwa ni hatua ya kujibu mapigo dhidi ya vikwazo ilivyowekewa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tayari Mrekani imewawekea vikwazo viongozi 11 wa ulinzi wa Urusi.

Mbali na Urusi kuwazuia viongozi hao wa Marekani, Taifa hilo limetangaza kuzuia mali zao zilizomo nchini humo.

Kwa mujibu wa Mtandao wa BBC Swahili, taarifa ya vikwazo hivyo imetolewa jana Jumanne na Wizara ya Mambo ya Nje Urusi.


 
Ikizungumzia vikwazo ilivyowekewa nchi yake na mataifa ya nje ikiwemo Marekani, kufuatia hatua yake ya kuivamia kijeshi Ukraine.


Joe Biden, Rais wa Marekani
Mbali na Rais Biden, maofisa wengine wa Marekani waliowekewa vikwazo hivyo, ni Katibu wa Ikulu ya Marekani, Antony Blinken. Katibu wa Ulinzi, Lloyd Austin. Katibu wa Habari, Jen Psaki. Mwenyekiti wa Wakuu wa Wafanyakazi, Mark Milley.

Wengine waliowekewa vikwazo ni Mshauri wa Taifa hilo wa masuala ya Usalama, Jake Sullivan na naibu wake Daleep Singh. Mismamizi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Samantha Power. Naibu Katibu wa Hazina, Wally Adeyemo na Rais wa Benki ya Export-Import ya Mrakeni, Reta Jo Lewis.


Marekani ni miongoni mwa mataifa ya nje yaliyiwekea vikwazo vya kiuchumi Russia, ambapo mataifa ya magharibi yamemuwekea vikwazo Rais wa Urusi, Vladimir Putin. Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavron na Katibu wa Habari, Dmitry Peskov.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad