3/17/2022

Vita nchini Ukraine: Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu kuizingira Kyiv

Mbele ya jengo la ghorofa lililoharibiwa baada ya kushambuliwa kwa roketi huko Kyiv mnamo Machi 17, 2022.
Mbele ya jengo la ghorofa lililoharibiwa baada ya kushambuliwa kwa roketi huko Kyiv mnamo Machi 17, 2022. AFP - GENYA SAVILOV
Katika siku ya 22 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Alhamisi Machi 17, nchi saba za Magharibi zikiwemo Ufaransa, Marekani na Uingereza zimeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zikiituhumu Urusi kwa "uhalifu wa kivita".

Joe Biden alimwita Vladimir Putin "mhalifu wa kivita", baada ya ukumbi wa sinema uliokuwa na raia huko Mariupol kushambulia, kulingana na manispaa ya jiji hilo. Huko Kyiv, mtu mmoja ameuawa katika shambulio na kuwajeruhi watatu.

Pointi kuu:
► Nchi saba za Magharibi (Uingereza, Marekani, Albania, Ufaransa, Norway na Ireland) zimeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi mchana kuhusu Ukraine kutokana na kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini humo.

► Vladimir Putin, rais wa Urusi, "ni mhalifu wa kivita" kulingana na Joe Biden, rais wa Marekani. Kremlin imeyachukulia matamshi haya kuwa "hayakubaliki na hayawezi kusamehewa".


 
► Mamlaka ya Ukraine inashutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia Jumba la Kuigiza la Mariupol, jiji lililozingirwa, wakati "zaidi ya watu elfu" walikuwa wamekimbilia huko. "Hatutawahi kusamehe hili", inahakikishia manispaa kwenye Telegram. Idadi ya watu bado haijabainishwa.

► Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu kuzingira mki mkuu wa  kyiv

► Siku ya Jumatano, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa, iliamuru Urusi kusitisha uvamizi wake nchini Ukraine.

► Baraza la Ulaya limeitenga rasmi Urusi kwa sababu ya vita vilivyoanzishwa dhidi ya Ukraine

Wakati huo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, limesema litatoa kundi la kwanza la kofia 125  za chuma na fulana za kuzuia risasi zenye nembo ya "vyombo vya habari" ili "idadi kubwa zaidi ya waandishi wa habari wanaofanya kazi nchini Ukraine wawe na vifaa hivi muhimu", kama sehemu ya hatua za dharura za kulinda waandishi wa habari wanaoripoti mzozo huu.

Tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, waandishi wa habari watano - watatu kutoka Ukraine, Mfaransa mwenye asili ya Ireland, Mmarekani - wameuawa. "Kila siku, waandishi wa habari na wanataaluma wote wa vyombo vya habari huhatarisha maisha yao nchini Ukraine ili kuwajuza wakazi wa eneo hilo na ulimwengu mzima ukweli wa vita hivi", amebaini Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger