Zungu amtoa hofu Rais Samia kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu amemtaka Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, asiwe na hofu kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025, akisema wananchi wanampenda. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Zungu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 7 Machi 2022, akizungumza katika ziara ya Rais Samia kwenye Shule ya Sekondari ya Benjamini William Mkapa, jijini Dar es Salaam.

“Usiwe na hofu kuhusu uchaguzi unaokuja 2025, wananachi wote wanakupenda. Hawawezi kukupenda wote lakini wengi wanakupenda na wengi wamekubali na kwa dua za vijana hawa na dua za masheikh na wachungaji wetu mambo yatakwenda kuwa mazuri,” amesema Zungu.

Aidha, Zungu amesema Rais Samia amefanya jambo ambalo watangulizi wake, marais wastaafu, Hayati Benjamini William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete na Hayati John Pombe Magufuli, hawakulifanya, la kukutana na wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


 
“Kwa mujibu wa historia ya nchi yetu ni mara ya kwanza Rais ambaye yuko   katika madaraka anakutana na wanafunzi kama hawa leo, nilianza kazi zangu za siasa 2000, wakati Mzee Mkapa akiwa Rais hakufanya, JK hakufanya na hayati JPM hakufanya lakini wewe umefanya,” amesema Zungu.

Wakati huo huo, Zungu amemuomba Rais Samia aiboreshe Dar es Salaam, kwa kuiboreshea mazingira mazuri ya kiuchumi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu katika maeneo ya wafanyabiashara hasa Karikaoo na Upanga.

Aidha, amemuomba Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, asimamie mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), awamu ya tatu, ili miundombinu ya jiji hilo ikamilike.


“Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo unachangia mfuko mkuu wa Serikali kwa asilimia 75 mpaka 80, ukiliboresha Jiji la Dar es Salaam unaiboresha Tanzania , uchumi wa Dar es Salaam ukitetetereka nchi nayo inaweza kutetereka,” amesema Zungu na kuongeza:

“Nikuombe Rais maeneo ya Kariakoo, Upanga na maeneo yote ambayo kuna biashara, biashara nyingi zimepungua sababu miundombinu sio mizuri, lakini jitihada zinafanywa nakushuru sana.Waziri wa Fedha achangamkie fursa ya DMDP awamu ya tatu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad