4/21/2022

Afande Sele: Tulipeleka mahari kwa Maunda ZorroMsanii Afande Sele ameshea kwamba kabla ya kifo cha Maunda Zorro alipeleka mahari kwa Mzee Zahir Zorro kwa ajili ya mdogo wake kutaka kumuoa lakini bahati mbaya akafariki.
Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Afande Sele amesema kwamba

"Maunda Zorro mimi ni familia yangu, mahari yake nimepeleka kwa Mzee Zorro na Banana Zoro, tukawakabidhi pesa tukisubiri harusi lakini kwa bahati mbaya M/mungu kafanya kazi yake".

Pia ameongeza kusema aliongea na Maunda wiki moja kabla ya kifo chake ambapo walipanga kusherekea pamoja sikukuu ya Pasaka.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger