4/10/2022

Ahmed Ally awatuliza Mashabiki Simba SCMeneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Polisi Tanzania yanapaswa kusahauliwa kwa haraka na Mashabiki/Wanachama wa klabu hiyo.

Simba SC leo Jumapili (April 10) ilicheza ugenini Uwanja wa Ushirika- Moshi Mkoani Kilimanjaro na kuambulia matokeo hayo ambayo si rafiki kwa Mashabiki na Wanachama wake.

Ahmed Ally amewataka Wanachama na Mashabiki kupotezea matokeo hayo kupitia andiko alilolichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya Kijamii.

Ahmed Ally ameandika: ✍️ @ahmedally_

Si matokeo ya kufurahisha hata kidogo lakini tunapaswa kuyasahau haraka na akili yetu sasa tuielekeze kwenye jambo kubwa lilolo mbele yetu Robo fainali dhidi ya Orlando Pirates


 
Najua tumeumizwa na matokeo haya lakini hatuna budi ya kuyapokea na kuheshimu juhudi za mpinzani wetu

Watu wenye akili timamu hawatumii muda mwingi kujadili kilichopotea baadala yake ni kuwekeza nguvu kupigania kile kilicho mbele yetu

Tunarejea Dsm leo hii kuanza maandalizi ya mchezo wa Jumapili ijayo dhidi Orlando


Poleni sana wana Simba wenzangu na tugange ya jayajo🙏🙏

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger