4/18/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Simba vs Orlando"1:WOW.. WHAT A MATCH🙌 Tumeshuhudia dakika 90 za viwango vya Juu. Mechi bora. Mechi Dume. Mechi yenye hadhi ya Robo Fainali ya AFRIKA

2: Tumeona Vita ya Mbinu kwenye Mabenchi ya Ufundi. Tumeona vita ya Ufundi kiwanjani 🙌 Kipindi cha pili, INTENSITY ya Mechi ilipanda ikawa Burudani kwa mpenzi wa soka bila kujali unashabikia Timu gani..

3: Tactically, Orlando walianza na mfumo 4-3-3 wakiwa kwenye Low Block Defensive System. Ubora wao kwenye kuubana uwanja uliwapa Simba maswali magumu sana.. Umbali kati ya mstari mmoja wa ulinzi kwenda mwingine.. Umbali kati ya mchezaji mmoja kwenda mwingine ilionyesha jinsi Orlando walivyo 'Master' home work yao kucheza Ugenini dhidi ya Simba

4: Naelewa kwanini PABLO alianza na viungo wawili wa chini.. Kwa Daraja la Orlando huwezi kuanza mechi kwa 'Kujilipua'. Sapraiz ambayo naamini hakuitegemea ni jinsi Orlando walivyo switch game ya kipindi cha pili. Kivipi?

5: Orlando walirudi na kucheza kwenye High Line! Wakatoka nyuma. Tactically hapa ndipo mahala ambapo BWALYA alihitajika uwanjani. Game ilifunguka na Simba wakaanza kutumia mapana ya uwanja.. 'Sub' zilikuwa sahihi ishu ni QUALITY ya walioingia

6: Kama kuna pigo Simba limewaathiri Simba kiufundi ni kuumia kwa BEN MORRISON. Nafikiri kwa uzoefu wake, ubora wake kwenye kushinda 1v1, zile ni nyakati ambazo Simba walihitaji sana hatua zake kiwanjani

7: Moja katika jambo ambalo Pablo anatakiwa kulitegemea kwenye mchezo wa marudiano ni ILE KASI ya Orlando kipindi cha pili. Kazi ya kwanza kwenye Uwanja wa mazoezi ni kutafuta Unit zile ili waweze kudhibiti presha ya Ugenini..

8: Yule Deon Hotto anajua sana! Guu lake la kushoto lilimfanya Kapombe awe na Tahadhari sana.. Game ya Marudiano, akiungana na Lorch na Gabadinho Mhango, Kasi ya mchezo itapanda zaidi

9: HENOCK BAKA.. SUPER DEFENDER🙌 Alikuwa Timamu kwenye kucheza mipira ya juu. Timing yake kwenye kusoma mipira inayotumwa nyuma ya mgongo wake iliwapa Simba nguvu sana kwenye safu ya Ulinzi

10: Nilipenda sana utulivu wa Refa kwenye maamuzi yake👏 Well Done KAPOMBE.. Well Done Mkude.. PETER BANDA wakati ambao Simba walimuhitaji ndio amewaangusha

Nb: Wameshinda Lakini hawana raha 😃

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger