4/30/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona YANGA vs SIMBA"
1: DAKIKA 180 za KARIAKOO DERBY BILA BAO, KWENYE LIGI MSIMU HUU. Ni Derby iliyotunyima Bao Lakini imetupa Jibu la Ubingwa wa NBC PREMIER LEAGUE.. Yanga watasherehekea Kombe lao, Simba watabaki na Heshima yao

2: Tactically, Makocha wote walikuwa na wasiwasi kwenye mipango yao. Ni kama waliwaza zaidi hatima zao baadae kuliko pointi 3 mbele ya Mtani .. Kivipi?

3: Timu zote zilikwenda na mfumo wa 4-2-3-1 Lakini Tofauti ikawa kwenye utekelezaji tu. Yanga wakaseti mtego wao kwenye Counter Attack.. Simba wakatafuta pasi mpenyezo nyuma ya ukuta wa Dickson Job na Mwamnyeto.. Wapi walifeli?

4: Moloko hakuwa kwenye Form yake. Hakuweza kutumia faida ya Mayele kusimama katikati ya Henock na Onyango.. Simba walikosa 'Movements' za Mugalu ili kutengeneza nafasi kwenye 'Half Spaces' ili Sakho na Morrison kutumia

5: Kuna funzo Henock na Onyango wamelitoa kwa mabeki wengine jinsi ya kudeal na Mayele. Kivipi? Jinsi ya kuziba nafasi ya nyuma ya mwenzako.. Asilimia kubwa Mayele alijikuta anafanya 'mikimbio' yake katikati ya Mabeki wawili wa Simba.. Ikapunguza kabisa madhara yake

6: Heshima kwa Shomari Kibwana✊ Mwili wa Primary, Ukatili wa Guantanamo Bay! What A Kid. Ameicheza 'Derby' kwa miguu, kichwa na Moyo wake. Ujasiri wake.. Kasi na Timing nzuri ya kupokonya mpira, iliwapa Yanga nguvu kwenye kujilinda

7: Mkude..👏 Ukitafuta kwa makini nini kilipunguza ukali wa Feisal kwenye 'zone ya 14' ya kiwanja anaposhambulia.. Utaiona kazi kubwa ya Jonas Mkude.. Sio kwa ajili ya kukata. Ni kwenye 'Brain' ya kukaba zone

8: YANGA wamecheza Dakika 90 bila Shot On Target. Why? Kuna ubora wa Pablo Tactically kwenye kujilinda Lakini kwa kiasi fulani Uongozi wa Yanga umejua ni Quality gani ya kuongeza kwenye kikosi chao kudeal na 1v1

9: Well Done Ramadhan Kayoko na Wasaidizi wake. Kiasi fulani mechi ilikuwa na presha kubwa. Kama wasingekuwa Fit na makini, kadi zingeweza kuwa nyingi zaidi

10: Shomari Kapombe 👏 Mchango mzuri Muzamir Yassin! Hongera kwa Mwamnyeto na Dickson Job.. Mechi nzuri kwa Perfomance zao

Nb: Kumbe inawezekana bila kuwasha moto 😃

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger