4/15/2022

Aslay, Abby Chams na Young Lunya Wasainiwa na Rockstar Africa


Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, wasanii @aslayisihaka, @abby_chams na rappa @younglunya wamekaribishwa kwenye record label ya Rockstar Africa ambayo itakayokuwa inafanya nao kazi kama ambavyo imekuwa ikifanya kazi na Ommy Dimpoz.

Watatu hao ambao kwasasa wapo nchini Afrika Kusini, wamesaini na label hiyo kubwa Afrika kwaajili ya kusimamiwa kwa kazi zao za muziki. Rockstar Africa ni label inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.

Pia label hiyo nchini Tanzania ishawahi kufanya kazi na wasanii kama AliKiba, Lady Jay Dee na Baraka The Prince.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger