4/27/2022

Baba Levo "Harmonize Hawezi Mzima Diamond Platnumz"

 


#BABAlevo au Mtaalam Fundi Manyumba; ni msanii wa Bongo Fleva, komediani na mtangazaji wa Wasafi ambaye amemchamba msanii Harmonize kwa mara nyingine na kusema kwamba mkurugenzi huyo wa Konde Music Worldwide hana uwezo hata chembe wa kumzima Diamond Platnumz kwa lolote iwe kimuziki au hata kufanya kiki.

Kwa mujibu wa Baba Levo, #Harmonize bado hajai hata kwenye kiganja cha #Diamond au Mondi kwani ni kama mtoto tu anayejaribu kuiga baba’ke wa muziki, lakini ameshindwa na kuamua kutumia njia hasi ya kutembeza chuki na matusi dhidi yake mitandaoni badala ya kujitahidi kumfikia na akishindwa kumfikia basi arudi kujiunga naye na kumshabikia.


“Harmonize hana uwezo wa kutengeneza kiki ya kumfunika Diamond Platnumz, kwa vyovyote vile hana uwezo wa kuzima EP ya FOA,” anasema Baba Levo.


Chawa huyo wa Diamond au Simba anatilia mkazo kwamba amesema mara nyingi tu kwamba si Harmonize pekee, bali msanii yeyote atakayedanganyika akajaribu kushindana na Diamond, basi atapoteza vingi; yaani itakuwa kama ng’ombe anayejaribu kushindana na ndovu, bila shaka atakwama kwenye gogo la tembo.


“Nimeshasema mtu yeyote atakayejaribu kushindana na Diamond ataishia kupoteza vitu vingi,” anasisitiza Baba Levo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger