4/18/2022

Baby Madaha Adai Marehemu Maunda Aliomba Msaada wa Maombi Kabla ya Kifo Chake

 
Msanii wa Bongo Fleva Baby Madaha amemuongelea marehemu Maunda Zorro kama mtu aliyekuwa mwema enzi za uhai wake

MWANAMUZIKI wa zamani wa Bongo Fleva Baby Madaha ameongelea ukaribu aliokuwa nao na msanii ambaye kwa sasa ni marehemu Maunda Zooro.

Katika mahojiano kwenye kipindi cha Mapito kinachorushwa na 22globalradio na Global TV amedai maunda alikuwa na tatizo la kiimani ambapo siku mbili kabla ya kifo chake alimuambia kuwa hajisikii vizuri, kwani anaota ndoto za ajabu ajabu na akaomba kama itawezekana basi apate msaada wa maombi kutoka kwa mchungaji.

Baby Madaha anaendelea kwa kusema kuwa yeye pamoja na Meneja wake walifanya jitihada za kumuunganisha na Mchungaji na akafanikiwa kuongea naye kwa njia ya simu na kumuelezea changamoto alizopata ambapo mchugaji alipanga muda wa kuonana ili ampatie huduma ya maombi lakini ilipofika siku hiyo Maunda Zorro hakuweza kupokea simu.

Baby Madaha anadai Maundo aliomba msaada wa Maombi kutoka kwa mchungaji kabla mauti hayajamkuta

Kwa upande mwingine Baby Madaha amemuelezea marehemu Maunda Zorro kama mtu aliyekuwa na roho nzuri mchangamfu na mwenye upendo kiasi kwamba aliweza kuwa rafikiyake mkubwa na hadi sasa haamini kama kweli hayupo naye tena.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger