4/23/2022

Biharusi Aliyewawekea Wageni BANGI Kwenye Chakula AkamatwaDanya Svoboda biharusi ambaye anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kuwawekea wageni bangi kwenye chakula

DANYA SVOBODA ni bibi harusi ambaye yeye na mhudumu wake, Joycelyn Bryan wamekamatwa na Polisi huko Florida nchini Marekani baada ya kubainika ni kweli waliongeza bangi kwenye chakula ambacho kilitolewa kwa wageni wa harusi yake.

Mmoja ya wageni waalikwa katika harusi hiyo alitoa ushahidi kwa kusema; “Nilianza kuhisi tofauti baada ya kula, nilijisikia kama mlevi hivi…

“Nilimpomuuliza bibi harusi kama waliongeza bangi, akajibu ndiyo na akasisimka…”

Siku ya tukio hilo ilibidi maofisa wa Polisi kuitwa kwenye sherehe ya harusi hiyo kusaidia wageni ambao walisema walihisi kama walikuwa wamepewa dawa za kulevya na baadhi kupoteza fahamu.

Baada ya vipimo vya vyakula na vinywaji vya sherehe hiyo, viligundulika kuwa na chembechembe za bangi.

Madawa ya Kulevya aina ya bangi

Bibi harusi huyo pamoja na mhudumu wake wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya maamuzi ya kizembe na kulisha watu bangi bila ridhaa yao.

Huko Florida, inasemekana bangi ni halali kama ikitumika kimatibabu, lakini si kwa matumizi ya dawa hiyo kwa burudani, tofauti na katika baadhi ya majimbo ya Marekani.

Cc; @sifaelpaul

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger