Bosi Simba Afungukia Ujio wa VAR CAF Kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es SalaamUONGOZI wa Simba umefurahia ujio wa Msaada wa Video kwa Refa (VAR) itakayotumika kwa mara ya kwanza katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kutangaza kutumia VAR ambayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam itatumika kwa mara ya kwanza tangu uanze kutumika.

Simba wataanza kuitumia VAR katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini utakaopigwa Aprili 17, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema kuwa ni furaha kwao kwenda kuandika historia ya timu ya kwanza kutumia VAR kwenye uwanja huo.


 
“Simba tunakwenda kuwa timu ya kwanza kutumia mfumo wa msaada wa VAR kwenye Uwanja wa Mkapa hapa jijini Dar es Salaam.

“Ni jambo la kheri sana kuwepo kwa VAR uwanjani, nadhani mashabiki wa Simba wasubiri kupata burudani siku hiyo ya mchezo.

“Tayari Caf wameshatoa taarifa kuhusiana na uwepo wa matumizi ya VAR kwenye mchezo wetu wa kwanza wa robo kwenye uwanja huo,” alisema Mangungu.

Waamuzi watakaocheza mchezo huo wa kati ni Haythem Guirat kutoka Tunisia wasaidizi ni Khalil Hassani (Tunisia), Samuel Pwadutakam (Nigeria), Sadom Selmi (Tunisia), msaidizi wa video, Ahmed Elghandour (Misri) na msaidizi wa VAR Youssef Wahid Youssef (Misri).

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad