Brazil Wamtega Guardiola kwa Sh Bilioni 30 Kuifundisha Timu ya Taifa, Yupo Man City Hadi 2023IMERIPOTIWA kuwa Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amepewa ofa ya mshahara wa pauni milioni 10 kwa mwaka (Sh bilioni 30 na milioni 228) ili akubali kuifundisha timu ya taifa ya Brazil.

Brazil watakabiliwa na ushindani kwa kuwa Shirikisho la Soka la Uholanzi nalo linamwania kocha huyo mwenye miaka 51.

Guardiola ana mkataba na Man City hadi 2023 na inawezekana akamaliza miaka yake ya mafanikio klabuni hapo.

Kocha wa sasa wa Brazil, Tite, tayari ameshathibitisha kuwa ataondoka katika timu hiyo baada ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, na sasa Brazil inasaka mrithi wake.


 
Kwa mujibu wa Marca, chama cha soka cha Brazil kinaona Guardiola ndiye mtu sahihi anayetakiwa kuinoa timu yao ya taifa.

“Hatua inayofuata ni (kuinoa) timu ya taifa kama nitapata nafasi hiyo,” alisema Guardiola mwanzoni mwa msimu huu.

Alipoulizwa kuhusiana na timu ya taifa ya Brazil, Guardiola alisema: “Ni timu nzuri ya taifa. Daima Brazil ni chaguo sahihi. Ilikuwa na itaendelea kuwa.”


STORI: RIO DE JANEIRO, Brazil
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad