4/06/2022

Bumbuli Ajitapa "Azam FC watatuchangia YANGA Alama Sita Muhimu"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Klabu ya Young Africans Hassan Bumbuli anaamini iwe isiwe, msimu huu Azam FC watawachangia alama sita katika safari yao ya kusaka Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2021/22.


Tambo za Bumbuli dhidi ya Azam FC zimekuja, kufuatia mchezo utakaowakutanisha Kesho Jumatano (April 06) katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es salaam.


Bumbuli amesema wana uhakika kwa ubora wa kikosi chao, Ushindi utapatikana kesho Jumatano, na watajiongezea alama zaidi ili waendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.


“Huu Ndiyo msimu wa kwanza ambao Azam watatuchangia Alama 6 kwenda kwenye mbio zetu za ubingwa hatuna Shaka na hilo.” Amesema Bumbuli


Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 48 baada ya michezo 18 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama zake 28, saba nyuma ya Simba SC iliyopo nafasi ya pili.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger