Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM Dar yaomba Ilala igawanywe

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba amemuomba Makamu mwenyekiti wa CCM, Abdulrahmani Kinana kusaidia ufanikishaji wa kuigawa Wilaya ya Ilala ili kuwapunguzia kazi viongozi wa wilaya hiyo.

 Ametoa rai hiyo leo Jumapili Aprili 10, 2022 katika hafla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho katika Jiji la Dar es Salaam inayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Kamba amesema Wilaya ya Ilala ni kubwa na inaweza kutoa wilaya mbili hadi tatu jambo ambalo pia litawasogeza viongozi karibu na wananchi.

"Muone jinsi mkuu wa wilaya, Mkurugenzi anavyofanya kazi kutoka Ilala hadi Zingiziwa, kufanya hivi itawasaidia nao waende kwa speed kama Ubungo, Temeke, Kinondoni na itawafanya viongozi wawe karibu na watu wao,"


 
Ameswma anashukuru wilaya hiyo kubeba Jiji lakini imekuwa na mambo mengi.

"Lakini unaona, eneo hili pia ni Manispaa na kazi ya Kumbilamoto (Omary-Meya wa jiji) ni kubwa sasa tusaidiane ili kazi iende vizuri. Nimeona nichomekee hili kwa sababu wewe ni mpya unaweza kutusaidia.


Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amewahakikishi wananchi kuwa mafuta yapo ya kutosha na meli zingine zenye bidhaa hiyo zinaendelea kuwasili nchini.

Makalla amesema kazi ya Serikali ni kuhakikisha wanawabana wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kuificha bidhaaa hiyo ili iwe adimu.


“Mambo yako mengi lakini niseme suala la mafuta, kwamba kulitokea sintofahamu kwamba mafuta yamepanda bei, lakini kikubwa ninachotaka kuwahakikishia ni kwamba mafuta yapo ya kutosha NA MELI zingine ziko nyiani na zingine zitashusha” amesisitiza Makalla

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments