4/06/2022

Chama, Pablo wang'ara tuzo za March

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA
Kiungo wa klabu ya Simba Sc, Clatous Chota Chama ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi March katika NBC Premier league 2021/22 na kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Simba kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa msimu huu wa ligi.
Chama anakuwa mchezaji wa saba kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika ligi kuu huku kwa mwezi March akiwabwaga nyota wawili Fiston Mayele (Yanga) na Frank Kahola (Mtibwa Sugar ) waliongia kwenye kinyang'anyiro cha mwezi huo.

Upande wa tuzo ya kocha bora wa mwezi march imekwenda kwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc Pablo Franco ambaye ni mara ya kwanza na yeye kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi March wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC Premier league) 2021/22 baada ya kuwa na matokeo bora kwa mwezi huo .

Pablo aliiongoza Simba kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo miwili dhidi ya Biashara Mara United na dhidi ya Dodoma Jiji huku akiwashinda makocha wawili Nasreddine Nabi (Yanga Sc) na Francis Baraza ( Kagera Sugar) walioingia kwenye fainali ya mwezi March ihali tuzo ya meneja bora wa uwanja imekwenda kwa meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa ,Nsajigwa Gordon kwa kufanya vizuri kwenye michezo iliyofanyika kwenye uwanja huo kwa mwezi march na kulinda miundombinu ya uwanja kwa ujumla.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger