4/11/2022

Chris Rock Atoa Mpya "Sitaongea Sakata la Will Smith Kunipiga Kofi Hadi Nilipwe"


Mchekeshaji Chris Rock amesema hatozungumzia sakata la kuchapwa kibao na Will Smith hadi pale ambapo atalipwa pesa. Mchekeshaji huyo alizungumza hayo mbele ya wahudhuriaji wa onesho lake juzi Ijumaa, ambapo alisema

“Mimi niko sawa, nina hii show nzima, lakini sitaongelea kuhusu hilo hadi pale ambapo nitalipwa. Maisha ni mazuri, nimerudisha hali yangu ya kusikia.” alikaririwa Chris Rock.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, wameichambua kauli hiyo na kusema kwamba pengine Chris Rock anataka kulipwa pesa ndefu kwa ajili ya kufanya mahojiano maalum kuhusu tukio lile. Au pia ana mpango wa kufungua kesi dhidi ya Will Smith ambapo atalipwa pesa ndefu.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger