4/21/2022

Diamond Platnumz Ashutumiwa Kubeba Nyota za WenzakeNiazime muda wako kidogo. Diamond, ni msanii mkubwa lakini namba zake za 'kolabo' na wasanii wa Kibongobongo ni ndogo. Ondoa wa WCB ambao kimsingi ni sehemu ya mbavu zake.

Ajabu ni kwamba hata wale wachache aliofanya nao kazi, wametoweka kisanii. Akigonga ngoma na msanii flan, huyo msanii hutoweka katika ramani. Hili liko wazi kabisa.

Shetta, ni wa mwanzo kufanya ngoma na Mondi. Lakini baada ya ngoma zile walizoshirikiana, Shetta akakaa nje ya ulingo. Siyo tena Shetta yule wa kabla ya kolabo yake na Mondi.

Chegge 'Mtoto wa Mama Saidi'? Dude la 'Waache waoane'? Bonge moja la ting'a, badala ya kumpa 'laifu tamu' Chegge, likampa talaka ya kwenda mafichoni.

Linex. Naye kiwese cha muziki kwenye 'tenki' lake kikakata. Baada tu ya kupiga dude na Mondi. Leo yupo kama hayupo. Kifupi hasomeki, wakati ngoma lilishika kinyama.

Nevy Kenzo, ile Kamata waliofanya na Mondi, badala ya kuwa ngazi ikageuka tiketi ya kuwatuliza. Hawajaweza tena kutoka na mtoko wa 'levo' ile. Kimya.

Shida ni nini. Au akishirikishwa, ngoma inaenda mbali na kugeuka msalaba kwa msanii? Kwamba anapata tabu ya kurudi na ngoma kubwa zaidi?

Ukiachana na Shetta, Chegge, Aika & Nareal 'Nevy Kenzo' na Linex. Ni msanii yupi aliyefanya naye ngoma kisha akatoweka? Hata Ney wa 'Muziki Gani' siyo huyu wa sasa.

Imeandikwa na @officialtinana

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger