Diamond Platnumz Atoa ya Moyoni "Huwa Nawaona Wanaonitukana Mitandaoni Ila Namwachia....."

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Diamond Platnumz; ni staa wa kimataifa wa muziki nchini Tanzania ambaye amefunguka juu ya watu wanaotambua mchango wake kwa nchi au la huku akiwaambia wanaomtukana Mungu anawaona.

Akihojiwa na mtangzaji Salim Kikeke kwenye Televisheni ya BBC Swahili, Diamond au Mondi anasema kuwa watu wanamtukana kiasi kwamba anashangaa ni kwa nini wanamtukana na kujiuliza amewafanya nini.

“Lakini nimegundua kuwa asilimia 99 ya wanaonitukana siyo kwamba wananichukia, lakini ni namna ya wao kujipatia riziki.

“Kiukweli mwanzoni nilikuwa ninapata hasira, lakini baadaye niliona ni kitu ambacho siwezi kukwepa kwa sababu nipo kwenye industry ya muziki.

“Mimi nikishaona tu kichwa cha habari nikashtuka, lakini ninajikontroo sana, ninachoangalia je, mauzo ya muziki wangu yanapanda? Nikiona hivyo najua tu ni chachandu na mengine ninamuachia Mwenyezi Mungu,” anasema Diamond au Simba.
Diamond au Mondi kwa sasa anaendelea kulikamata Bara la Ulaya wakati huu ambapo ana kampeni maalum ya kuitangaza albam yake fupi (EP) ya First Of All (FOA).
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad