4/23/2022

Fahyma Aupiga Mwingi Kwa Rayvanny "Mfikishieni Salamu kidudu Mtu"


Faima Msangi au Fahyma; ni baby mama wa staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny ambao mwaka mmoja baada ya kutengana, kuna ishara nyingi za kuthibitisha kwamba.

Taarifa hizo zimeanza kubamba wakati huu kukiwa na tetesi kwamba, Rayvanny au Vanny Boy ameachana na mpenzi wake mpya ambaye ni Paula Kajala; yule binti wa mwigizaji Kajala Masanja na prodyuza P Funk Majani.

Habari za ndani zinaeleza kuwa, kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo Fahyma ameendelea kutamba na kurusha vijembe kwamba yeye ni mzuri kuliko huyo mwingine.

MFIKISHIENI SALAMU KIDUDU-MTU
Mbali na vijembe pia Fahyma muda mwingi anasikiliza nyimbo za Rayvanny au Chui na msanii wake chini ya lebo yake ya Next Level Music (NLM), Mac Voice hasa zile zenye maneno ya kujimwambafai, kujiamini na kutamba kwamba amefanikiwa kumrejesha jamaa huyo na yupo naye sambamba akisema mfikishieni salamu yule kidudu-mtu, apunguze mashauzi na kujidai.

Vyanzo vya ndani vinadai kuwa, kwa sasa mpira umerudi kwa kipa ambapo Rayvanny na Fahyma walianza kuonekana wiki iliyopita katika kumbukizi ya kuzaliwa kwa mtoto wao, Jaydanny iliyofanya kwenye Mgahawa wa Havanna uliopo Mbezi-Beach jijini Dar ikielezwa unamilikiwa na Vanny Boy.

MAPENZI YA KWELI HAYAFI?
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya wafuasi wao wanasema wameamini ule msemo usemao ‘mapenzi ya kweli hayafi’ na hata yakifa hayaozi na hata kama ikitokea yakaoza, basi hutoa harufu ya marashi mazuri zaidi.
Fahyma na Rayvanny miaka kadhaa nyuma walipendana mno hadi wakafikia hatua ya kupata mtoto pamoja.

Lakini kwa bahati mbaya, baadaye walitengana huku sababu kubwa ikidaiwa ni usaliti na mwanamke kupenda maisha ya gharama kuliko uwezo alionao, hali iliyomfanya Rayvanny ahamishie majeshi kwa mrembo Paula Kajala; binti mdogo na mbichi.

PAULA AREJEA KIMYAKIMYA
Tofauti na alivyozoeleka, tangu Paula arejee kimyakimya kutoka masomoni nchini Uturuki, hajaonekana na Rayvanny huku Fahyma akiendelea kumsapoti jamaa katika kazi yake ya muziki.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger