4/12/2022

Familia ya Osinachi Nwachukwu mwimbaji injili Yakana Ndugu yao Kufariki Kwa Kansa, Mume Aangushiwa LawamaFamilia ya Osinachi Nwachukwu mwimbaji injili maarufu barani Afrika kutoka Nigeria, imekana ndugu yao kufariki kwa kansa ya koo bali imesema kifo chake kimesababishwa na unyama aliokuwa akifanyiwa na mume wake pichani 

Dada wa Osinachi akihojiwa amesema ndugu yao alikuwa akinyanyasika vibaya sana ndani ya ndoa kwa muda mrefu lakini akawa anawaficha hata wao wanafamilia.

Dada mtu amesema mume wa Osinachi pichani Peter Nwachukwu ambaye ni mwinjilisti alikuwa na roho ya kinyama sana kwa kumpiga kila wakati na kumnyima uhuru hata wa kuitembelea familia yake na wanafamilia..hata kijijini kwao aliruhusiwa kwenda mara moja tu tena wakati baba yao alipofariki 2017 na siku hiyo wakiwa ndani ya gari alimpiga pia mkewe ambapo ndugu yao mwingine aliona

Amesema kilichomuua ndugu yao ni kupigwa teke la kifuani na mumewe huyo na bado mume aliwaficha hata ndugu yao alipokuwa yupo hospitali na hata huyo mume mwinjilisti hospitalini hakumueleza daktari kuwa alimpiga mkewe teke la kifuani

Rafiki wa mume huyo ndie alimtaarifu pacha wa Osinachi kumuuliza je una taarifa kuwa ndugu yako yupo kwenye hali mbaya baada ya kupigwa teke la kifuani na mumewe, pacha wake akajibu hana taarifa. Daktari hospitali alithibitisha Osinachi kuvilia damu ndani kwa ndani kifuani kwake na baadaye kufariki

Dada wa Osinachi amesema ilifikia hatua wakamwambia ndugu yao kuwa hii sio ndoa tengana na huyo mume uendelee kuwa hai ili ulee wanao 4 mliozaa pamoja, lakini Osinachi akawa anasema atabadilika na pia kusema Mungu hapendi talaka, ndugu zake wakamwambia tenganeni tu ubaki kulea wanao sio talaka na kutengana sio dhambi yeye akawajibu atabadilika 

Dada yake amesema kiujumla huyo mume wake hakuwa na mawasiliano mazuri na wanafamilia wote akiwemo mama yao na kaka yao, ndugu walizuiwa kuwa karibu na Osinachi na huyo mume alishajua mapema mke wake kafariki lakini alikaa masaa mengi yakapita ndio akapiga simu kuwataarifu mama wa Osinachi na Kaka wa Osinachi ambao hakuwa na mawasiliano mazuri nao kwa muda mrefu, na walipopigiwa simu mama.wa.Osinachi akamwambia ndicho ulichokuwa ukikitaka hadi afe kisha huyo mume akamkatia simu mkwe wake huyo

MALIZIA PART 2....  

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger