4/11/2022

Fiston Mayele Ataja Waliomshawishi Kuja YANGA, Agusia Kuishia Masaki Kwenye Jumba la Kifahari


"Kisinda na Mukoko ndio walinishawishi nije Yanga, sana Kisinda aliniambia kuna shida ya Straiker Yanga naomba uje akanipa namba ya Eng Hersi mkataba wangu ulipoisha AS Vita nikamtafuta Hersi tukaongea tukasaini Mkataba wa Miaka miwili.

Niliwaambia Viongozi wa Yanga wanitafutie nyumba ambayo itakuwa na sehemu ya Gym, naishi Masaki kila asubuhi nafanya Mazoezi yangu halafu jioni naenda Avic Town kwa ajili ya Mazoezi ya Timu.

Mapokezi yamekuwa Makubwa Watu wananipenda style yangu imekuwa maarufu hadi makanisani, Watanzania wanapenda sana Mpira Upendo wanaonioshesha Yanga unanifanya niendelee kupambana kwa ajili ya Timu hii"-Fiston Mayele.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger