4/16/2022

Yaliyomkuta R Kelly yamgeukia Trey SongzKesi mpya inamshutumu Trey Songz akihusishwa na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na ubakaji, iliwasilishwa kwenye vyombo vya dola huko Los Angeles nchini Marekani siku ya Jumanne, ambapo mwathiriwa aliyemshtaki Songz, amefahamika kwa jina la ‘Jane Doe’.

Katika hati za mahakama zilizopatikana, kufuatia tukio hilo mwanamke huyo anahitaji kulipwa fidia ya dola milioni 20.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halisi halikutajwa anadai kuwa alikuwa na uhusiano wa kawaida wa ngono mara kwa mara na mwimbaji huyo nyota mwenye umri wa miaka 37, lakini anadai kuwa mambo yalibadilika Machi 24, 2016 alipombaka kinyume na maumbile.

Hati za mahakama zinasema kuwa alidai kwamba alihitaji na kupokea huduma ya matibabu ya dharura mara moja baada ya tukio hilo, ambalo alisema kuwa lilifanyika wakati wa tafrija huko West Hills Calfonia.


 
Mlalamikaji anadai Songz, ambaye jina lake halisi ni Tremaine Neverson, aligeuka kuwa mbakaji mara tu walipoingia chumbani ambapo mwanamke huyo anadaiwa alipiga kelele kwa uchungu na kumsihi mwimbaji huyo kumuacha, bila mafanikio.

Muda mfupi baadae mwanamke huyo anadai alitoroka nyumbani mara tu baada ya shambulio hilo, na anasema dereva wake wa Uber alimpeleka katika hospitali iliyo karibu kwa vile hakuwa akijihisi vizuri Kulingana na alichofanyiwa, alifika katika Kituo cha Afya cha Providence Joseph Kitengo cha Huduma ya Dharura usiku wa manane mnamo Machi 25.

Anadai kuwa madaktari walimwambia kwamba alikuwa ameathirika kwa kiasi katika sehemu zake za siri, athari ambayo ingehitaji kufanyiwa upasuaji kutokana na shambulio hilo.


Mwanamke huyo alisema katika nyaraka za mahakama kwamba hakuwapa polisi wanaochunguza tukio hilo jina la Songz kwa sababu alikuwa katika mshtuko na kuhofia maisha yake.

Mwathiriwa anadai kuwa amepatwa na mfadhaiko wa kihisia, ambayo anasema imemfanya kuwa na woga, wasiwasi, fedheha, huzuni, na majeraha mengine ya kimwili na ya kihisia, yakiwamo madhara ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi.

Licha ya kesi hiyo nzito inayomkabili Songz, inaelezwa kuwa mpaka sasa mwanamuziki huyo amekwisha shitakiwa na jumla ya wanawake watatu tofauti kwa utovu wa nidhamu na unyanyasaji wa kingono.

Jambo hilo linatengeneza taswira ya masuala yaliyomkuta mwanamuziki  nyota na nguli wa R&B duniani R Kelly ambaye mpaka sasa anaendelea kutumikia kifungo kwa makosa yanayoshabihiana na anayotuhumiwa nayo Trey Songz.


 
Wakati R Kelly akihudumu katika kifungo chake zinaenea fununu za kuwa mwimbaji huyo anatengenezewa Makala maalumu itakayoangazia masuala yake yote hasa yaliyohusisha unyanyasaji wa kingono kwa wanawake, makala inayoaminika kuwa pengine ndio likawa kaburi la nyota huyo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger