Ghasia zakumba Uswidi kufuatia tukio la uchomaji wa Quran

Maelezo ya picha, Maaandamano yaliendelea siku ya Jumapili katika mji wa Norrköping
Ghasia zimeendelea kushuhudiwa kwa siku ya nne katika miji kadhaa ya Uswidi, kufuatia hatua ya kuchomwa kwa nakala za Quran iliyofanywa na kundi la mrengo wa kulia, linalopinga wahamiaji.

Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa watu watatu walijeruhiwa katika mji wa Norrköping mashariki mwa nchi siku ya Jumapili baada ya polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya waandamanaji.

Magari kadhaa yamechomwa moto na karibu watu 17 kutiwa mbaroni.

Siku ya Jumamosi, magari kadhaa ikiwemo basi moja yaliteketezwa katika mji wa kusini wa Malmo wakati wa mkutano wa kundi la mrengo wa kulia.

Awali, serikali za Iran na Iraq zilitoa wito kwa wajumbe wa Uswidi kukemea uchomaji huo.

Rasmus Paludan mwenye msimamo mkali na mzaliwa wa Denmark- Uswidi, ambaye anaongoza vuguvugu la Stram Kurs (msimamo mkali), alisema amechoma maandishi matakatifu ya Uislamu na angerudia tena kitendo hicho.

Takriban maafisa 16 wa polisi waliripotiwa kujeruhiwa na magari kadhaa ya polisi kuharibiwa katika machafuko ya siku ya Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi katika maeneo ambayo kundi la mrengo wa kulia lilipanga matukio, ikiwa ni pamoja na viunga vya Stockholm na katika miji ya Linköping na Norrköping.Polisi walisambaratisha umati wa waandamanaji katika eneo la Rosengård huko Malmo siku ya Jumamosi
Maelezo ya picha, Polisi walisambaratisha umati wa waandamanaji katika eneo la Rosengård huko Malmo siku ya Jumamosi
Paludan alikuwa ametishia kufanya mkutano mwingine huko Norrköping siku ya Jumapili, na kusababisha waandamanaji kukusanyika hapo, Deutsche Welle iliripoti.

Polisi wa eneo hilo walisema katika taarifa kwamba walifyatua risasi za onyo baada ya kushambuliwa na watu watatu wanaonekana kupigwa na risasi bandia.

Mkuu wa polisi wa kitaifa wa Uswidi Anders Thornberg alisema katika taarifa yake Jumamosi kwamba waandamanaji wameonyesha kutojali maisha ya maafisa wa polisi, na kuongeza: "Tumeona ghasia kali hapo awali. Lakini hili ni jambo lingine."

Maandamano ya kupinga mipango ya Stram Kurs ya kuchoma Qur'ani yamewahi kuzua vurugu nchini Uswidi. Mnamo 2020, waandamanaji walichoma moto magari na maduka kuharibiwa katika mapigano huko Malmö.

Paludan - ambaye alifungwa kwa mwezi mmoja mwaka 2020 kwa makosa kadha ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa rangi nchini Denmark - pia amejaribu kupanga uchomaji wa Quran katika nchi nyingine za Ulaya, ikiwemo Ufaransa na Ubelgiji.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad