4/13/2022

Gwiji wa Mchezo wa Basketball Duniani Ajutia Kuikataa Dili ya NIKE Enzi Kampuni Ikiwa ChangaGwiji la mchezo wa Kikapu duniani Magic Johnson amefunguka ya moyoni kwamba anajutia kuwahi kuipiga chini dili ya NIKE na kusaini na kampuni ya Converse. Kwenye mkutano na Waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa filamu ya Winning Time: The Rise of the Lakers Dynasty, Magic Johnson amesema sasa hivi angekuwa Trilionea kama angesaini na NIKE wakati ule.

Dili hiyo ilienda kama ifuatavyo; Mwanzoni mwa miaka ya 1980, kampuni ya Converse ilimpa ofa ya ($100k) zaidi ya TSh. 232M kwa mwaka wakati NIKE ambayo ilikuwa bado ni kampuni changa ilimpa ofa ya ($1) kwa kila kiatu kitakachouzwa pamoja na kumpatia hisa 100,000 za kampuni hiyo ambapo hisa 1 ilikuwa ikiuzwa kwa ($0.18)

Magic Johnson ambaye ni nembo ya Los Angeles Lakers, hakuona faida ya hisa kwa wakati huo hivyo akaamua kuchukua pesa yake taslimu toka Converse, leo inakadiriwa kuwa alipoteza kiasi cha ($5 Billion) zaidi ya TSh. Trilioni 11.6 kwa kuikataa dili ya NIKE.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger