Hatimaye Baba Levo afichua jina la 'mke' wa Diamond, si Zuchu





Diamond Platnumz na Baba Levo
Msanii Baba Levo baada ya kuwatata mashabiki waweke ‘comment’ zaidi ya elfu mbili ili akalitoboe jina la mpenzi mpya wa bosi wake Diamond Platnumz, hatimaye hajafeli kwani amedokeza jina hilo.

Kupitia Instagram yake, Baba Levo alidokeza kwamba herufi A ni miongoni mwa herufi katika jina hilo la ‘mke’ wa Diamond kwa kusema kwamba huenda herufi hiyo ikawa ya mwanzo au ya mwisho katika jina hilo, kikubwa ni kwamba ipo kwenye jina.


 
“Herufi A inaweza kuwa ya mwanzo au ya mwisho kwenye jina lake. Mshamjua au niongeze herufi?” aliuliza Baba Levo.

Bila shaka kwa ufichuzi huu kama si mawenge anachezea mashabiki na wafuasi wa Diamond basi dhana mbalimbali zinaweza zakajieleza bayana.

Moja ya dhana ambayo inajotokeza hap ani kwamba moja kwa moja msanii Zuchu rasmi hayupo katika orodha ya wale ambao walikuwa wanapigiwa upato wa kuingia kwenye pango la Simba huyo wa WCB, kwani katika jina lake, hamna ja herufi A mwanzo au mwisho au hata kwenye jina lenyewe.

Baada ya sema sema nyingi mitandaoni kuhusu uwezekano wa Diamond na Zuch kuwa katika mahusiano, hatimaye Baba Levo amewatia breki wale waliokuwa wakieneza uvumi huo katika ufichuzi wake kwamba jina la mpenzi wa Mond lina herufi A.

Hapa mashabiki na wafuasi wa Simba wanazidi kujikuna vichwa zaidi huku baadhi wakilazimika kuchepuka kutoka mkondo wa Zuchu na kuingia mkondo tofauti wa Aaliyah, mtangazaji katika kituo cha Wasafi ambaye pia wiki hii ametajwa kuwa ndiye huenda akawa mke wa Diamond.

Ila kama ilivyo ada, mambo mazuri hayataki haraka, kwa hiyo tulia, kaa mkao wa kula na chukua ‘popcorn’ zako kwani ndio mwanzo mkoko unaalika maua. Mbivu na mbichi itajulikana hata kabla ya mwezsi mtukufu wa Ramadhani kukamilika.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA



 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad