4/26/2022

Hatimaye Channel ya Youtube ya Msanii Diamond Platnumz imerejea Tena Hewani


Hatimaye channel ya youtube ya msanii @diamondplatnumz imerejea tena hewani katika mtandao wa youtube baada saa kadhaa kuondolewa na youtube wenyewe.

Channel hiyo ambayo ina siku mbili tangu idukuliwe (hacked), mapema leo ilikuwa imeondolewa na youtube (terminated) kufuatia kukiuka masharti na kuvunja sheria zilizowekwa na youtube.

Mkuu wa Kitengo cha Digital katika kampuni ya WCB, @kimkayndo mapema leo alifunguka sababu za youtube kuiondoa channel hiyo, ambapo alisema; "Kutokana na live iliyoruka siku ya Jumapili pindi channel hiyo ilipokuwa imehakiwa na kutoa maudhui yaliyovunja sheria za Youtube" alieleza @kimkayndo kupitia ukurasa wake wa twitter.

✍️: @omaryramsey


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger