4/30/2022

Hawa Hapa Wachezaji wa Kuchungwa Kwa Pande Zote Mbili...Wakizubaa tu Watu Wanalia

 


TAKWIMU za mechi sita zilizopita za Ligi kwa kila timu, zinatoa taswira kuwa wachezaji wanne wenye majukumu ya kushambulia watakuwa katika ulinzi mkali wa ukuta wa wapinzani wakati Yanga na Simba zitakapoumana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, leo Jumamosi.

Nyota hao wanne ni washambuliaji Medie Kagere na Fiston Mayele pamoja na viungo washambuliaji, Saido Ntibazonkiza na Clatous Chama kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwa kuzifungia mabao, timu hizo mbili katika mechi sita zilizopita za Ligi.


Ukuta wa Simba ambao kuna uwezekano mkubwa ukaundwa na kipa Aishi Manula na mabeki Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Enock Inonga na Joash Onyango, utakuwa na shughuli pevu ya kuwadhibiti nyota wa Yanga, Mayele na Ntibazonkiza.


Katika mechi sita zilizopita, ukuta huo wa Simba umeruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja tu lakini Jumamosi watakutana na kibarua cha kuwakabili Mayele na Ntibazokinza ambao katika mabao 12 ambayo Yanga imefunga katika mechi sita zilizopita, wao wawili kwa pamoja wamefunga mabao nane huku mengine manne yakipachikwa na wengine.


Mayele ndio tishio zaidi kwa safu ya ulinzi ya Simba kwani yeye pekee amefumania nyavu mara sita huku Saido akifunga mabao mawili na kiujumla mchango wao kwa pamoja katika mabao yote 12 ambayo Yanga imeyapata katika michezo hiyo ni 66.67%.


Ikumbukwe kwamba katika mechi sita mfululizo zilizopita za ligi, Mayele pekee amehusika katika mabao nane ya Yanga akifunga saba na kupiga pasi moja ya mwisho huku Ntibazonkiza akihusika na mabao manne, akifunga mawili na kutoa asisti za mabao mawili.


Lakini wakati ukuta wa Simba ukiwa na mtihani wa kuhakikisha Mayele na Ntibazonkiza hawafui dafu, upande wa pili nao watapaswa kufanya kazi ya ziada kuwatuliza mshambuliaji Medie Kagere na kiungo mshambuliaji Clatous Chama.


Ukuta huo wa Yanga kama hakutotokea majeruhi au changamoto nyingine, bila shaka utaundwa na kipa Djigui Diarra ambaye mbele yake watakuwepo mabeki Djuma Shaban, Kibwana Shomary, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.


Wawili hao ndio wamekuwa roho ya Simba katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu kwani kwa pamoja wamechangia zaidi ya nusu ya mabao yote tisa ambayo timu hiyo imeyafunga kwenye idadi hiyo ya michezo. Chama na Kagere wamefunga mabao sita. ambayo ni sawa na 66.67%

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger