Imebainika: Ombi la Mwisho la Mwai Kibaki Kabla ya Kukata RohoImebainika: Ombi la Mwisho la Mwai Kibaki Kabla ya Kukata Roho
Rais Mstaafu Mwai Kibaki anaripotiwa kuwa na ombi la mwisho kwa familia yake kabla ya kukata roho.
Kabla ya kukimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Nairobi Jumatano, Aprili 20, Kibaki aanaripotiwa kuwa na ombi la umoja kwa familia yake, kwa mujibu wa mwanawe mkubwa Jimmy Kibaki.

“Mkuwe kitu kimoja na mlinde wajukuu wangu,” Jimmy anasema hilo ndilo lilokuwa ombi la mwisho la babake aliyefariki mnamo Ijumaa ya Aprili 22 akiwa na umri wa miaka 90.

Akizungumza na familia yake kabla ya kukimbizwa hospitalini, Kibaki aliwasisitizia kuwa iwapo watatimiza ombi lake la mwisho basi watakuwa wamemtia furaha pamoja na mke wake Lucy katika maisha yao ya baada ya duniani.


 
Vita vya Uhuru na DP Ruto Vyajitokeza Katika Misa ya Wafu ya Kibaki
Katika muhula wake wa pili na wa mwisho, Kibaki alionekana mara kadhaa na wajukuu wake katika Ikulu ya Rais.

Baada ya kustaafu, wajukuu wake walikuwa kando yake katika boma lake la Muthaiga kila wakati shule zikifungwa.

Kwa mujibu wa wanawe, baba yao alikuwa na ukaribu sana na watoto. Mjukuu mkubwa zaidi wa Kibaki ana umri wa miaka 26.


Jimmy Kibaki anasema kuwa babake alikuwa mtu aliyependa unadhifu na alihakikisha kuwa ameiacha familia yake katika hali nzuri.

Ameliahidi taifa kuwa familia hiyo haitashuhudia mizozo kwa inayotokana na mali za baba yao kama inavyoshuhudiwa katika familia zingine mashuhuri.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad