4/06/2022

Jay Z Anavyozidiwa Utajiri Kwa Kasi na Vijana Aliowatengeneza Mwenyewe , Rihanna na Kanye West

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAShawn Corey Carter a.k.a Jay Z ni moja ya marapa wenye heshima kubwa duniani na ni miongoni mwa watu walioplay part kubwa kwenye Mafanikio ya wasanii wengi nchini Marekani wakiwemo Rihanna na Kanye West (Ye) na habari kubwa kwa sasa kuhusu watu hawa ni namba za utajiri wao kwa mujibu wa Jarida la Forbes.

2002 Record Label ya ROC A FELLA ya Kwake Jay Z na wenzie wawili ilimsaini rasmi Kanye West kama Producer wakihofia kumpoteza baada ya kufanya kazi kali nyingi kwa muda mrefu bila mkataba,lakini moyoni Ye alikuwa anatamani kuwa Rapper,angefanya nini wakati Label nyingi zilimkataa kumsaini maana hakuwa na muonekano wa kigangstar kama ilivyokuwa kwa wasanii wengi wa Hip Hop. Lakini pia ni producer aliyetengeneza hits kwenye albamu ya Jay Z, Blueprint 2001, 2002 Ye alipata ajali,akiwa hospitalini alitumia muda huo kutengeneza wimbo “through the wire ” na hapo safari ya kuwa rapa ikaanza na kuachia albamu yake ya The college Dropout,huku akipewa backups kubwa na Jigger.

2003 Jay Z alimsaini Rihanna na wakatengeneza hit inayoitwa Umbrella,ikawa ni mikwaju baada ya mikwaju. Kuna uvumi unadai wawili hawa waliwahi date lakini kwa siri sababu Rihanna alikuwa chini ya umri 🔞,na Jigga alikuwa na Beyonce,lakini Jigga kaplay part kubwa sana kwenye career ya Riri.

Licha ya Jay Z kuwa ndiye Rapa ama msanii wa kwanza kuwa Billionaire,(2019) lakini kwasasa amekuwa msanii wa 3 nyuma ya Rihanna na Kanye West akiwa na utajiri wa $1.4B, Rihanna ametajwa na forbes kwa mara ya kwanza kama Billionaire akiwa na Dollar za kimarekani 1.7B huku utajiri wa Kanye West ukipanda hadi Dollar za kimarekani 2B.

The Family on the one table.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger