4/13/2022

Jeshi la Polisi Lakamata Dawa za Kulevya zilizokuwa Zimefichwa Kwenye Chaja za Simu Uwanja wa Ndege Dar

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA


Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam limewakamata Watuhumiwa watano wa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya kati ya March 17,2022 hadi April 08,2022 ambapo kesi nne za kusafirisha dawa za kulevya zimefunguliwa.

"March 17,2022 tulikamata kifurushi kikiwa na chaja saba ambazo sita zilikuwa na unga mweupe Gramu 234.54 ndani yake wa Methamhetamine uliotumwa toka Afrika Kusini, tayari Watuhumiwa wawili wakazi wa Singida mmoja Raia wa China na Mtanzania wamekamatwa wakihusishwa na dawa hizo za kulevya"

"April 04,2022 tulimkamata Raia wa Tanzania (42) aliyewasili Aiport akitokea India akiwa amemeza pipi mbili za Cocaine zenye uzito wa Gramu 34.79"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger