4/30/2022

Odemba Adaiwa Kumbemenda Msanii wa Konde Music Ibraah, Afunguka MapyaMwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania mwenye umri wa miaka 40, Miriam Odemba.
Miriam Odemba; ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania mwenye umri wa miaka 40 ambaye amegonga vichwa vya habari akidaiwa kumbemenda msanii wa Konde Music, Ibrahim Abdallah Nampunga almaarufu Ibraah mwenye umri wa miaka 23.

Hii ni baada ya hivi karibuni Odemba kukiri kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Ibraah.

Kwa upande wake Odemba amejitokeza hadharani na kujibu shutuma hizo akisema kuwa, uhusiano wake na Ibraah ni wa kirafiki tu.

Odemba anasema kuwa alijuana na Ibraah kupitia bosi wa Konde Music Worldwide, Harmonize.


 
“Kwa kweli Ibraah ni rafiki yangu. Ni kupitia Harmonize nimemjua Ibraah. Napenda sana muziki wake. Ni mdogo wangu, ananiheshimu na ananipenda sana,” anasema Odemba.


Odemba anaeleza kuwa, kwa kawaida Ibraah humchukulia kama dada yake mkubwa.

“Ananipenda mimi kama dada yake. Ndiyo maana kuna kipindi alinipa namba yake ya simu, lakini nikawa simpigii simu.


“Kuna siku alinipigia simu nikawa nimefurahi. Nilifurahi na kusema kwa kweli mdogo wangu kanikumbuka,” anasema Odemba ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Kwa upande wake, Ibraah aliliambia gazeti hili kuwa, ni kweli Odemba ni rafiki yake wa karibu, lakini hakuna kingine cha zaidi akimaanisha siyo wapenzi.

Stori; Khadija Bakari, Dar

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger