Ticker

6/recent/ticker-posts

Kajala Amfanya Harmonize Akeshe Mazoezini

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Harmonize au Konde Boy Mjeshi; ni supastaa wa Bongo Fleva ambaye anakiri kwamba inapotokea mhuni akampenda mwanamke mrembo, basi ni noma, IJUMAA linaripoti.
Harmonize anakiri kwamba, mwanamama Kajala Masanja au Mama Pau amemfanya ashinde na kukesha kwenye ‘gym’ akifanya mazoezi.

Hii ni baada ya kugundua kwamba, mwigizaji Kajala anapenda kufanya mazoezi ya gym na amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu sasa tangu mwanzoni mwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa Kajala, amefanikiwa mno kupunguza ule mwili wake mkubwa na sasa amekuwa mwepesi na mwenye mwonekano wa kuvutia.

HARMO AFANYA KILA LIWEZEKANALO
Sasa; baada ya kugundua hilo, Harmonize au Harmo ambaye amekuwa akifanya kila linalowezekana ili Kajala amsamehe na kurudisha penzi lao hivyo naye ameingia gym kupunguza mwili na kujiweka fiti akiamini labda mwanamama huyo atavutiwa naye na kumlegezea kamba.

Juu ya upendo wa Harmonize kwa Kajala, hakuna mwenye shaka kwani jamaa huyo amekuwa hapoi wala haboi ili tu kumlainisha mwanamama huyo.
Kwa mujibu wa Harmonize, sababu ya kuingia gym kwenye mazoezi ni kwa sababu ya Kajala ambaye amemvutia kuwa mtu wa mazoezi.
Konde Boy anasema kuwa, yote anayofanya ni kutokana na Kajala.

HARMO: MHUNI AKIPENDA!
“Amenifanya kuwa mtu wa mazoezi, nyie mhuni akipenda! Mwanamke wangu ndiye mshawishi wangu…” Anasema Harmonize.

Hii inaonesha ni jinsi gani penzi lake kwa Kajala limemvutia Harmonize zaidi, lakini pia ufanyaji wa mazoezi wa mwanamama huyo umemvutia jamaa ili aende naye sawasawa ili kumuonesha mapenzi ya hali ya juu aliyonayo kwake.

Katika kumshawishi Kajala amrudie, Harmonize amekuwa akifanya mambo kedekede ambapo mwishoni mwa mwezi Machi, aliweka bango lake na mwigizaji huyo katika eneo la Kinondoni-Manyanya jijini Dar.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments