Kajala na Harmonize Watu Ndio Tatizo Penzi lao
Harmo katangaza zawadi kibao. Kubwa kuliko zote ukiacha bango ni lile Range Rover. Usawa huu kuihonga pisi ndinga ile lazima uwe na roho ngumu. Na pisi kuikataa Range ni ujasiri wa kiwango kisichopimika.

Any way. Pengine kosa la Harmo ni kubwa kiasi cha kutosameheka (ingawa haiwezekani). Na huenda ukubwa wa kosa ndo unafanya atangaze hongo ovyo. Brother Pesa haijawahi kuwa suluhisho la hisia za mwanamke.

Lakini pia kuna watu nyuma ya jambo la hili. Ambao msingi huenda wakawa ndo sababu kuu ya msamamo wa Kajala. Na kumpotezea jumla Mmakonde wa watu (masikini). Watu ni sumu ya mbinge za mapenzi.

Wapo wanaomsapoti Kajala kwa upendo wa kweli. Pia na wanaomsapoti kwa choyo, wanajifanya wapo na Kajala. Lakini moyoni hawataki kuona akipush gari kali mjini. Hawa ndo wengi zaidi.

Wanasimama naye kwa mtazamo wa akose. Yaani wanafurahia anavyoikataa Range ili aendelee kusukuma Nadia sijui Raum kama wao. Kundi hili wapo wa karibu na wa mbali, hao utawaona kwenye comment insta.

Wapo wanaoogopwa na Kajala. Yeye anataka asamehe ajibebee Rover, ila wazazi, marafiki na jamii itamtazamaje? Inategemea na sababu alizotoa kwao za kumpiga chini na Konde. Hili lipo sana kwenye mapenzi.

Kwa ujumla sakata hili linaendeshwa na watu. Maisha ya kioo yanaumiza sana. Sisi tunaweza kuamini kuwa Konde Boy anaumia sana, kumbe kinyume chake Kajala ndo anasumbuka zaidi na macho ya watu.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad