Kifo cha Padri Dar; Polisi wasema kuna dalili amejiua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




SAKATA la kifo cha Padri Francis Kangwa (49) raia wa Zambia aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yohanne Paul II, iliyoko Mbezi Mshikamano wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, limezidi kuchukua sura mpya baada ya Jeshi la Polisi mkoani humo kudai kuwa uchunguzi wa awali unaonesha dalili kwamba Padri huyo anaweza kuwa amejiua. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Padri Kangwa ambaye alifariki dunia Aprili 12 mwaka huu, mwili wake ulikutwa ndani ya tenki kubwa la maji lililopo nyuma ya nyumba ya makazi ya Mapadri iliyopo mtaa wa Sokoine katika jengo la Ottoman jijini Dar es Salaam.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 19 Aprili, 2022 na Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salam- ACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.

Amesema uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi unaonesha dalili kwamba Padri huyo anaweza kuwa amejiua.

Aidha, amefafanua kuwa Padri huyo alifika katika kanisa la “St. Joseph” lililopo mtaa wa Sokoine tarehe 12 Aprili 2022 kwa ajili ya ibada maalum na mara baada ya ibada alielekea kwenye makazi ya Mapadri kujipumzisha lakini hakuonekana mpaka tarehe 15 Aprili 2022 alipokutwa amefariki eneo hilo.

Hata hivyo, Jeshi hilo limesema linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi iliyopelekea kifo cha Padri huyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad