4/13/2022

Kijana Alieoa Mwanamke Mzee wa Miaka 70 Afunguka Mkewe Huyo Kuwa Fiti KitandaniPichani Benard Musyoki(35) amesema watu wamekuwa wakimuuliza kama huwa anakutana faragha kwenye tendo la ndoa na mke wake huyo mzungu kwa jina la Deborah(70) kwani umri umempa kisogo, ambapo amejibu kuwa ndio wanakutana faragha kama wanandoa wengine na ukweli mke wake huyo yupo kimahaba sana na nguvu zaidi za kuhimili vishindo vya mchakato husika hadi yeye mwanaume inamuwia vigumu kuendana na muziki wa mkewe huyo kunako sita kwa sita. Amesema mke wake huyo ana miaka 70 lakini yupo imara kama ana miaka 29

Ikumbukwe, Benard awali, Jamaa huyo alishasema kuwa kabla ya kumuoa mrembo huyo pichani toka Marekani amvapo walikutana Facebook, alishawahi kuwa kwenye mahusiano na wanawake watatu tofauti ambapo mahusiano hayo yaliishia kuangukia pua. Wanawake wawili wa mwanzo aliokuwa nao wote walikuwa Wakenya,

mwanamke wake wa tatu alikuwa mzungu pia kutoka Ujerumani mwenye miaka 50 walikutana pia Facebook mwaka 2016 ambapo jamaa huyo alikuwa akilipiwa bili zote na mzungu husika na kununuliwa pikipiki na baiskeli na huyo mzungu ila baadaye penzi lao likamomonyekeana kila mtu akala njia yake

Haukupita muda mrefu hukohuko Facebook ndio akamuopoa huyu Deborah(70), alimuomba urafiki Deborah kisha akamuambia nimekupenda tufunge ndoa hata will hazikupita wawili hao wakala viapo vya ndoa huko inbox, Facebook. Benard alitaka kwenda Marekani kumfuata Deborah ila akanyimwa visa, baada ya muda Deborah akaja yeye Kenya

Wazazi Deborah walifariki miaka mingi iliyopita kwahiyo suala la mahari ilibidi Benard alijadili na watoto wa Deborah ambao analingana nao umri. walimwambia alipe mahari ya shilingi 100 za Kenya ambazo ni sawa na elfu 2000 ya Tanzania kisha wakamwmabia Benard akaitoe sadaka kanisani mahari hiyo akafanya hivyo


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger