4/29/2022

Kocha Nabi ' Kesho Tutaingia Uwanjani Kibabe'UONGOZI wa Yanga umesema timu yao itashuka dimbani kivingine tofauti na ilivyozoeleka ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuvuna pointi tatu dhidi ya watani zao, Simba katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika mechi hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi alisema licha ya kutokuwa sehemu ya mchezo huo, atamaliza mikakati yake mazoezini kwa kuwapa mbinu za kiufundi 'mpya' ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

Nabi alisema anafurahi kuona wachezaji wake wote wako kamili kucheza mchezo huo na sasa anaendelea kuwaimarisha kwa kuwaongezea mbinu tofauti ambazo hazifahamiki.

"Nina uhakika wa kumkosa mchezaji mmoja pekee katika timu yangu, Yacouba Sogne, lakini wengine wote wako tayari kwa mchezo, nina kikosi kamili nafikiri kutakuwa na mabadiliko madogo katika kikosi kulingana na mbinu tutakazoingia nazo katika mchezo huo," alisema na kuongeza.


"Tuna nafasi kubwa ya kuchagua watu bora ambao tutawaona wako tayari kutupa ushindi, hii mechi tunatakiwa kushinda kwa namna yoyote, licha ya mchezo huo kuwa mgumu kwa sababu ya wapinzani wetu Simba wako vizuri na wametoka kucheza michuano ya kimataifa," alisema Nabi.

Aliongeza kwa sasa bado hajapata mwanga wa kiungo gani anaweza kuanza katika kikosi cha kwanza kwa sababu kila mmoja anafanya vizuri katika mazoezi na kuhakikisha kuwapo na mabadiliko katika nafasi hiyo.

"Nahitaji kupata ushindi katika mchezo huu, kuna kazi ya kuchagua mawinga wa pembeni ambao watakuwa na kasi kulingana na uchezaji wa mpinzani wangu Simba anavyocheza," alisema kocha huyo.


Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alisema msimu huu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatwaa ubingwa lakini pia watapenda kuona mashabiki wakijitokeza kwa wingi katika mchezo huo wa kesho.

“Kulingana na ukubwa wa mechi hiyo tunaomba mashabiki wajitokeze kwa sababu tunadhamira ya kushinda mchezo wa Jumamosi,” alisema Msolla.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger