Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha wa Simba Atoa Tamko Zito “Orlando Wazuri, Lakini Hawatoki kwa Mkapa”

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>KOCHA Mkuu wa Simba Mhispania, Pablo Franco amesema kuwa ni kweli wapinzani wao Orlando Pirates ya Afrika Kusini ni wazuri, lakini hatakubali wawafunge kwenye uwanja wa nyumbani.


Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Championi Jumatano, Pablo alisema kuwa licha ya ubora walionao Orlando lakini anaamini watafuzu hatua ya nusu ya michuano hiyo, kwani nao wapo vizuri.


Pablo alisema kuwa, wamefuzu hatua ya robo ya Shirikisho, kundi lao likiwa na timu bora mbili ambazo ni RS Berkane na Asec Mimosas.


Aliongeza kuwa hivi sasa wanakwenda kukutana na timu bora zaidi kwao ambayo ni Pirates, hivyo yupo katika maandalizi ya nguvu katika kuelekea mchezo huo ili apate matokeo mazuri ya ushindi.


“Tumefuzu robo fainali Shirikisho, kundi letu lilikuwa na timu mbili bora zaidi yetu, na sasa tunakutana na timu bora zaidi yetu ambayo ni Pirates.


“Hivyo basi nimefanya na ninaendelea ya nguvu ya kukiboresha kikosi changu ili kifanye vema katika mchezo huo wa kwanza ambao tutakuwa nyumbani.


“Niwaombe mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani wakati tutakapopambana dhidi ya Pirates, kwani sapoti yao ni muhimu katika kuhakikisha tunawafunga wapinzani wetu,” alisema Pablo.


Stori: Wilbert Molandi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments