4/18/2022

Kukosa Utulivu Ndani ya Lebo ya WCB, Huenda Rayvanny Alishaondoka Katika Lebo Hiyo Kitambo, Afuta Utambulisho WaoSTAA wa Bongofleva ambaye pia ni Mmiliki wa rekodi lebo ya Next level Music, Raymond Mwaikyusa ‘Rayvanny’ ameendelea kuibua minong’ono kuhusu kujiondoa kwake katika lebo Wasafi Classic Baby (WCB) baada ya kufuta utambulisho wa lebo hiyo katika akaunti yake ya Instagram. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Licha ya Wasafi kuwa lebo mama iliyomkuza kimuziki msanii huyo ambaye bado anajitambulisha kuwa yupo chini ya uongozi wa lebo hiyo, sasa amefuta Wasafi iliyokuwa ikimtambulisha kama mmoja wa wasanii wa lebo hiyo.
Maneno ambayo ameyaondoa kwenye bio yake ni yale yaliyokuwa yakisema “Signed under WCB WASAFI” na sasa bio yake hiyo imebaki kutawaliwa na maneno kama “CEO NLM MUSIC” pekee.

Kwa muda mrefu sasa baada ya msanii Harmonize kuvujisha maongezi baina yake na Rayvanny kuhusu sakata la kipindi alipokuwa akiondoka Wasafi, Rayvanny amekuwa akionekana kukosa utulivu ndani ya lebo ya Wasafi.

Mara nyingi amedaiwa kuonesha ishara za kutoka japo uongozi wa lebo hiyo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki imekuwa ikikanusha madai hayo.

Harmonize aliporejea nchini kutoka katika ziara yake ya kimuziki nchini Marekani, alivujisha maongezi yake na Rayvanny peupe mbele ya waandishi wa habari.

Yalikuwa ni maongezi ambayo Rayvanny alisikika akimtetea Harmonize dhidi ya vitendo vya bosi wao Diamond Platnumz na kumsema Simba vibaya kwamba hakuwa anamfanyia Harmonize fadhila kipindi akiwa chini ya Wasafi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger