Kumekucha..Simba SC yapiga marufuku Tochi Uwanja wa Mkapa

 


Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC imepiga marufuku Tochi za miale ya kijani, ambazo zimekua zikitumiwa na Mashabiki kuwamulika wachezaji wanapokua kwenye makujumu yao Uwanjani.


Simba SC imepiga marufuku Tochi hizo, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Jumapili (April 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Mashabiki wa Simba SC wanapaswa kuacha mpango wa kuingia na Tochi hizo, ili kuinusuru klabu yao kutozwa faini na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.


“Mchezo wetu uliopita dhidi ya USGN, baadhi ya Mashabiki waliingia Uwanjani na hizi Tochi licha ya kupiga marufuku, Simba kama taasisi na kama klabu hatupendezwi na utamaduni huu, ambao sio utamaduni wetu,”


“Simba SC ina utamaduni wake, sio huu ambao baadhi ya wenzetu waliuchagua katika mchezo uliopita, tunawaomba sana Wanasimba wote huu mpango wa kuja na Tochi uachwe mara moja, ili kuinusuru klabu yetu kuingia kwenye kadhia ya kutozwa faini na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’. Amesema Ahmed Ally alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu (April 11).


Simba SC ilitinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’ kwa kishindo, kufuatia kisago kilichoishukia USGN ya Niger cha 4-0 Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


Simba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USGN ya Niger zikitupwa nje ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad