'Kuachika kuna raha,'Paula Kajala asema baada ya uvumi wameachana na Rayvanny

Fununu zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii ni kwamba penzi kati ya msanii Rayvanny na mpenzi wake Paula kajala limekata Kamba baada ya misukosuko ya muda mrefu.

Inasemekana hatimaye wawili hao wametengana, picha kufutwa na kuacha kufuatana kwenye mtandao wa Instagram ambapo sasa ukitazama vizuri katika orodha ya watu anaowafuata Rayvanny, Paula hayupo pale hali ya kuwa siku za nyuma alikuwa miongoni mmwa watu waliokuwa wakifuatwa na msanii huyo.

Kwa upande wa mwanadada huyo pia ni vivyo hivyo ambapo baada ya kuenda masomoni Uturuki, Rayvanny alikuwa mpweke sana na pengine ndio sababu ya kulitamatisha penzi lao.

HUku Paula akizungumia swala hilo alidai kwamba kuachwa kuna raha yake, hivyo basi ina maana kwamba wawili hao wayuko pamoja, na kwamba Rayvanny ndiye aliyemuacha.


 
"Kuachika nako kuna raha yake asikwambie mtu,nilivaa adi nguo za chui chui lakini wapi 😭😭😭," Paula Aliandika.

Je wameachana au ni kiki tu wawili hao wanatafuta,baada ya Rayvanny kuondoka kwenye lebo ya muziki ya WCB, ni swali ambalo limesalia akilini mwa wanamitandao wengi, kwani wasanii wamezoea kutafuta kiki ili vibao vyao vifume.

Juzi kati Rayvanny aliungana na aliyekuwa mpenzi wake Fahyvanny kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe ambapo wapenzi hao wa zamani walimsherehekea kwa msururu wa picha safi na jumbe maalumu.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad