4/09/2022

Kutana na Mbunge Anayemiliki SIMU 19 Kwa Mpigo na Zote Zina Umuhimu


Mbunge wa eneo la Kesses nchini Kenya Mishra Swarup amekiri ni kweli anamiliki simu 19 za mkononi na zote anazitumia katika matumizi ya kila siku na kwamba kila moja ina nafasi yake muhimu katika shughuli zake za kutunga sheria, ujasiriamali na familia.

“Nina simu 19 sasa... na ninazitumia zote, nyingine ni za biashara, nyingine ni kwa ajili ya Wananchi na nyingine ni za uhusiano wangu wa kisiasa na kikazi kuwasiliana pia China, India, ambia na Congo, nina simu kwa ajili ya mama yangu, Baba yangu, Rais wangu, Naibu Rais wangu, Raila Odinga wangu, mimi na Mke wangu pia."

Mishra ambaye anatetea kiti chake cha Ubunge kama Mgombea huru kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya August mwaka huu alionesha pia iPhone yake ambayo anadai imetengenezwa kwa dhahabu safi na almasi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger