4/30/2022

Kwa Mkapa Hapatoshi Unaambiwa Shughuli imeanza Kufana Mapema

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPAZIMEBAKI zaidi ya saa saba, kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba kupigwa saa 11:00 jioni ya leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwenye maeneo ya nje ya Uwanja kuna mashabiki wa timu hizo mbili wakiendelea kununua tiketi na wengine wakipata chakula na vinywaji wakijiandaa kwa mechi hiyo.

Mashabiki wengine wa timu hizo mbili wapo kwenye makundi mbalimbali kuna waliokaa wa timu moja na wengine kuchanganyika huku kukiwa na mabishano ya kila mmoja akiamini timu yake inashinda.

Nje ya uwanja kuna wauza vyakula, vinywaji na bidhaa mbalimbali wakiendelea kufanya biashara kutokana na mashabiki wanaondelea kujitokeza Uwanjani hapo.

Kwenye mageti ya kuingia Uwanjani kuna mistari ya mashabiki mbalimbali wa timu hizo waliokuwa wamevalia jezi ya klabu zao pamoja wakisubiri mageti kufunguliwa saa 5:00 asubuhi ili kuingia ndani.

Kwenye barabara za kuingia Uwanja wa Mkapa kuna magari mbalimbali ya mashabiki wa timu hizo nao wakiendelea kumiminika huku kuna yaliondikwa matawi ya hapa Dar es Salaam na mengine nje ya mkoa kama Njombe, Mbeya, Songea na mengineyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger