4/16/2022

Liverpool Moto Chini, Yatinga Fainali ya Kombe la FA Kwa Kuichapa Man City


LIVERPOOL YATINGA FAINALI YA KOMBE LA FA - Liverpool imeendelea kupambania nia yake ya kutwaa mataji manne msimu huu baada ya kuingia fainali ya Kombe la FA kwa kuifunga Manchester City goli 3-2 katika Uwanja wa Wembley

Liverpool ambayo tayari imeshachukua Kombe la Carabao, inasubiri kuchuana na mshindi wa mechi kati ya Chelsea na Crystal Palace kwenye fainali ya FA. Bado ina uwezo wa kuchukua Kombe la EPL na Klabu Bingwa Ulaya

Katika Mchezo wa leo, Sadio Mané amekuwa Mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga goli mbili katika Nusu Fainali ya Kombe la FA tangu afanye hivyo Robbie Fowler dhidi ya Aston Villa mwaka 1996

Manchester City imekuwa timu ya pili kuondolewa katika hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya FA kwa misimu mitatu mfululizo baada ya Manchester United kufanyiwa hivyo kuanzia msimu wa 1963-64 hadi msimu wa 1965-66

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger