4/23/2022

Loui Aweka Rekodi South Africa , Wimbo Wake Wapata Hadhi ya Platnum Nchini Afrika Kusini


Msanii toka kwenye kiwanda cha muziki Tanzania @iamloui_ ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza toka Afrika Mashariki kuwa na wimbo uliofikisha hadhi ya Platinum nchini Afrika Kusini. Rekodi hiyo imewekwa kupitia wimbo (SELEMA) alioshirikiana na Musa Keys ambaye ni msanii na mtayarishaji toka nchini Afrika Kusini.

Leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari, mwimbaji huyo alituonesha Certificate ‘Plaque’ ambayo ametunukiwa na Recording Industry of South Africa (RISA) kwa mafanikio ya wimbo huo. Mafanikio ya wimbo huo sio tu kwenye vituo vya Redio na Televisheni nchini Afrika Kusini bali ni hadi kwenye majukwaa makubwa ya kununua na kupakua muziki mtandaoni kama Spotify ambapo una zaidi ya Streams 3M.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger