4/13/2022

Madam Flora Awafungukia Walio Katika Ndoa za Manyanyaso


Madam Flora mwimbaji injili maarufu Tanzania awafungukia walio katika ndoa za manyanyaso katikati ya taharuki kubwa iliyotanda juu ya kifo cha Osinachi aliyenyanyaswa na mume wake

"Unakaa kwenye ndoa kwa kuigiza una furaha lakini umejaa madonda mwili mzima kwa kipigo, Kuchanwa na viwembe n.k,
mama Mmoja alikuwa anapigwa na mumewe na ikafika mahali akapata tatizo la akili akapelekwa wodi ya vichaa,
mwingine alipigwa hadi akaharibiwa kizazi hawezi Kuzaa tena, waliopata ulemavu wakiwa kwenye ndoa na wengine kufa kabisa ni wengi hawaelezeki.

Swali langu.! Kifo kinachotakiwa kuwatenganisha ni kipi? Ni hiki cha kuteswa na mtu uliyedhani ni sahihi kufunga naye ndoa au ni kifo cha mapenzi ya Mungu.?
Kwanza unapokuwa unatendewa unyanyasaji huwezi kuwa na amani, muda wote moyo unakuwa na uchungu na maumivu, inapotokea kipigo cha siku hiyo kinaondoa uhai wako basi hata Mbinguni huingii pamoja na uvumilivu wako wa miaka 20 ya ndoa. Unakufa ukiwa na hasira, uchungu, mbingu gani Utaenda.?

Mungu amekupa akili na Maarifa zitumie vizuri
Bora ufe kwa mapenzi ya Mungu na sio kuifia ndoa isiyotambulika hata Mbinguni.
Kila mmoja atabeba furushi lake Hakuna ndoa inayoingia mbinguni ila ni mtu na Kiloba cha matendo yake.

Usisubiri ufe uache watoto wanateseka na mama wa kambo, mapenzi yapo tu angalia Usalama wako kwanza mengine Mungu atafanya.
Sio kila ndoa ni mapenzi ya Mungu ndoa nyingi ni za matamanio.
Kilicho cha Mungu hata Mkipishana ni rahisi kusameheana na upendo kutawala.

Kuna ndoa ikitokea mwanaume anashituka usiku Hana Shuka ila mkewe kajifunika tayari ugomvi, mke anaanza kupigwa akiwa usingizini kisa shuka.

Wanyanyasaji wa kijinsia wote Mungu anawaona haya machozi ya mnao wanyanyasa ndo yanakwamishwa hata maendeleo yenu.
Mwanamke jitambue na ambao hamjaolewa #msikurupuke
Ifike mahali Wanawake acheni unafiki saidieni wanawake wenzenu
Usifurahi mwenzako anaponyanyaswa kijinsia maana kesho yako huijui"

Kumbukumbu zinaonesha wakati wa gogoro la ndoa yake na Emmanuel Mbasha jamii ilionekana kumtuhumu zaidi Flora ila hakugeuka nyuma aliendelea na ustaarabu wake kuachana na ndoa hiyo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger