4/06/2022

Majaliwa Kassim "Simba Wanaupiga Mwingi Sana"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim leo Bungeni Dodoma ameipongeza Club ya Simba kwa kuupiga mwingi na kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

"Nitumie fursa hii kuendelea kusisitiza umuhimu wa michezo kwa kuvipongeza vilabu vyetu vya mpira wa miguu vinavyoshiriki kwenye mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) na Ligi Kuu Zanzibar (PBZ Premier League), hakika kwa mpira mzuri wanaocheza wanakonga mioyo ya washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu nchini"

"Kipekee niipongeze timu ya Simba Sports Club kwa kupeperusha bendera ya Taifa letu katika mashindano ya Shirikisho la Klabu Afrika, mwenye macho haambiwi tazama, sote tumeshuhudia wakiendelea kuupiga mwingi na kutuwakilisha vema katika medani za kimataifa"

"Niwapongeze pia wachezaji mahiri wa vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu vikiwemo Yanga (Timu ya Wananchi); Simba (Wekundu wa Msimbazi) Namungo (Wauaji wa Kusini), Azam (Wazee wa Lambalamba) Biashara United (Wanajeshi wa Mpakani), Dodoma Jiji (Walima Zabibu), Tanzania Prison (Wajelajela) na bila kuwasahau Mtibwa Sugar (Wakata Miwa na Kagera Sugar / Wanankurukumbi) Vilevile, nivipongeze vilabu vya Zanzibar vikiwemo KMKM, Mlandege, Malindi, Mafunzo na vilabu vinginevyo" ——— Waziri Mkuu @kassim_m_majaliwa
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger