Ticker

6/recent/ticker-posts

Mama Chris Rock Afunguka “Nimefurahishwa na Jinsi Mtoto Wangu Alivyoweza Kumudu Hali ile Bila kKuonyesha Hasira"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Mama mzazi wa mchekeshaji Chris Rock amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu tukio la mtoto wake kupigwa kofi na mwigizaji Will Smith katika halfa ya Tuzo za Oscar mapema mwaka huu.

Kupitia mahojiano exclusive na Wistv, Mama huyo amesema kitendo cha Will Smith kumpiga kofi mwanae ni kama alipiga vibao familia nzima.

“Alipompiga kibao Chris, alitupiga sote. Lakini alinipiga Mimi pia. Sijui ni kitu gani ningemwambia kama ningekuwa karibu yake, umemtandika mwenzako kibao, Hafikirii.” alieleza mama mzazi wa Chris Rock.

Aidha, Mama huyo amempongeza mwanae (Rock) kwa ujasiri aliouonesha mbele ya hadhira kufuatia ukomavu wake, “Nimefurahishwa na jinsi mtoto wangu alivyoweza kumudu hali ile bila kuonyesha hasira”.

Hata hivyo kwa upande wa mchekeshaji Chris Rock bado hajaweza kufunguka chochote tangu litokee sakata hilo huku ikidhaniwa kuwa anasubiri apate ofa au dili kubwa lenye pesa ndefu la kumfanya afunguke kuhusu tukio hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments