4/28/2022

Manara Akabidhiwa Rasmi Kadi ya Uanachama, Adai Ndoto Yake Imetimia

 


Mwenyekiti wa Yanga Dkt, Mshindo Msolla akimkabidhi kadi ya Uanachama Msemaji wa Yanga Haji Manara

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema hatimaye ndoto zake zimetimia za kuwa mwanachama wa Yanga hiyo ni baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama.

Katika tukio hilo, Haji Manara alikabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt, Mshindo Msolla huku akibainisha kuwa katika maisha yake ya kuwa ndani ya tasnia ya soka ikiwa ni pamoja na kuviwakilisha vilabu mbalimbali alivyofanyanavyo kazi hakuwahi kufikiria kuwa mwanachama wa klabu hizo.

Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari Manara ameelezea namna ambavyo alijiunga na Yanga kama msemaji lakini pia ameweka wazi namna mabyo anafanya kazi kwa ukaribu na Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Hassan Bumbuli.

Wakati anamkabidhi kadi ya uanachama, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dkt, Msindo Msolla amemuasa Manara kushirikiana na Bumbuli kuhakikisha kuwa wanawahamasisha wapenzi na mashabiki wa Yanga kujisajili na mfumo mpya wa kidigitali ili waweze kufanikiwa kutoka kwenye idadi ya wananchama hai walionao hadi sasa ambao wanakadiriwa kufikia milioni moja idadi iongezeke hadi milioni mbili.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger