4/26/2022

Manara "Inonga ni Beki Mzuri Tatizo Anapenda Kucheza na Jukwaa"Beki wa kati wa Simba Hennock Inonga akimsindikiza mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kufanyiwa mabadiliko
MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Sunday Manara akifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini amesema Beki wa kati wa klabu ya Simba Hennock Inonga ni bonge la beki akiwa na maana ni beki mzuri japo tatizo lake ni moja tu anapenda kucheza na jukwaa.

“Inonga ni beki mzuri lakini sijui shida yake inakuwa ni pi anapenda kucheza na akili za fans kuliko majukumu yake, kwa beki mzuri hawezi kufanya hivyo.

Kuna wakati anafanya jambo ili anufaishe mashabiki.”

Katika hatua nyingine kwenye mahojiano hayo Manara amewachambua baadhi ya wachezaji wa klabu ya Simba akiwemo golikipa namba moja wa klabu hiyo Aishi Manula, Beki wa Kulia wa Simba Shomari Kapombe, Beki wa Kushoto wa Klabu hiyo Mohamed Hussein pamoja na kiungo Jonas Mkude na winga wao Bernard Morisson akiwataja kuwa ni wachezaji wa daraja la juu.


Yanga namkaribisha Simba Aprili 30 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
Klabu ya Soka ya Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa wekundu wa msimbazi Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC mzunguko wa pili unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 30 mwaka huu

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger